WIKI YA CHANJO YAZINDULIWA NGORONGORO
24 April 2023
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Raymond Mwangwala Leo Aprili 24,2023 amezindua wiki ya chanjo Kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, chanjo zilizotolewani pamoja na chanjo ya kuzuia kupooza, kukinga surua, kukinga kuhara na magonjwa mengine.
Uzinduzi huo umefanyika katika kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro iliyopo kijiji cha Lopoluni kata ya Olorien Magaiduru ambapo wazazi wenye watoto wamefika na kupata chanjo hizo, watoto hao wamepewa chanjo kulingana na umri wa mtoto na kuzingatia aina ya chanjo ambazo mtoto alishapewa.
Watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 wamepewa chanjo ya kukinga saratani ya shingo ya kizazi.Pia wazazi wamesisitizwa kuitumia wiki hii kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo za magonjwa mbalimbali Ili waweze kuwakinga watoto wao
"Tuko kwenye maadhimisho ya wiki ya chanjo na sisi wan Ngorongoro tumeamua wiki hii tuiadhimishie hapa kwenye Hospitali lengo ni kuhakikisha Wananchi wa kata hii wanapata huduma hii na tunahakikisha zaidi ya Watoto 5000 watafikiwa na chanjo,niwapongeze wanafunzi wakike waliokuja kupata chanjo ya saratani, ugonjwa wa saratani ni hatari sana kwahiyo lengo la chanjo hii nikuwakinga watoto wetu na magonjwa yanayoweza kuzuilika" Mwangala amesisitiza kuwa chanjo hizo ni salama hivyo Wananchi wasione shaka kuwaleta watoto kupata chanjo
Katika uzinduzi huo ameshiriki Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Mohamed Bayo ambaye ameeleza kuwa kwa sasa huduma ya Afaya inapatikana karibia katika kila kata kuna kituo cha afya /Zahanati hivyo wananchi katika kipindi hiki ambacho tuko kwenye wiki ya Chanjo wajakikishe watoto kupata chanjo.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Emanuel Mhando amewapongeza wananchi wote waliowaleta watoto kupata chanjo hizo.
Mganga Mkuu wa Wilaya. Dkt Revocutus Dyekobora ameeleza kuwa Wiki ya Chanjo itaanza tarehe 24- 30 Aprili 2023 na itaongozwa na kaulimbiu ya "Tuwafikie wote kwa Chanjo na Ujumbe wa mwaka 2023 ni Jamii iliyopata chanjo ni jamii yenye Afya"
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.