Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe Raymond Stephen Mwangwala amewasihi wananchi wilayani Ngorongoro kuipokea kinga tiba na chanjo dhidi ya ugonjwa wa trakoma au vikope kwani in salama na inaufanisi wa kupunguza hatari ya upofu
Ameyasema hayo Leo tar 20/4/2023 wakati akizindua zoezi la utoaji chanjo dhidi ya TRAKOMA katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali teule ya Wasso ambapo zoezi hilo litaanza kwesho tar 21-28/4/2023 likihusisha watu wenye umri wa kuanzia miezi sita hadi watu wazima.
Mhe.Mwangwala amesema magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele yanaathiri jamii nyingi ambazo znakipato cha chini na huduma duni za afya hivyo kuisihi jamii kufanya udhibiti wa wadudu kama mbu,nzi na konokono wanaosambaza vimelea vya magonjwa haya na kufanya usafi wa mwili na mazingira.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuendelea kuienzi tunu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani mbali na mambo mengine umesaidia kuleta maendeleo kupitia mwingiliano wa kibiashara kati ya jamii mbalimbali kutoka pande zote za muungano huku akitolea mfano wa idadi kubwa ya wananchi wa jamii za Ngorongoro ikiwemo wamaasai ambao wapo wengi visiwani Zanzibar na wanaendelea kujitaftia riziki huku wakiendelea kudumisha mila huko waliko.
Kwa upande wake Bi.Florence Makunda mfamasia wa mpango wa NTDCP kutoka wizara ya afya kitengo cha magonjwa yaliyokua hayapewi kipaumbele amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk.Samia Suluhu Hassani alisaini makubaliano ya kimataifa yanayotaka hadi kufikia mwaka 2030 ugonjwa huu usiwe tatizo tena barani Afrika.
Akisisitiza kila kundi kuanzia wizara ya afya hadi ngazi ya jamii ikitekeleza wajibu wake ipasavyo jamii itafanikiwa kutokomeza ugonjwa huu
mkaazi wa Wasso bwana Maasai Juma ameishukuru serekali kwa kuleta kinga hii kwani itasaidia kupunguza matatizo ya macho huku akiwasihi wananchi wengine kuondoa hofu kua dawa hizi ni salama kwani ameshuhudia mkuu wa wilaya akimeza katika zoezi hilo la uzinduzi .
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.