Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Raymond Mwangwala leo tarehe 05 Novemba 2023 amehudhuria sherehe za kusimikwa rasmi Mch. Mathayo Loisulie kuwa mkuu wa jimbo kanda ya maasai kaskazini.
Aidha Mhe. Mwangwala amelipongeza kanisa kwa mafundisho ya upendo na amani yanayotolewa na kanisa hilo. Pia ametumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi serikali inavyoendelea kuchukua tahadhari kuhusu mvua zinazotarajiwa kunyesha.
"Niwaombe sana waumini, nikuombe sana askofu na timu yako tuomba muendelee kufanya maombi zije mvua zitakazotosheleza na zisiwe zisiwe mvua zenye madhara" alisisitiza Mhe. Raymond Mwangwala.
KKKT DAYOSISI ya kaskazini kati Jimbo la maasai kaskazini usharika wa Wasso umezinduliwa leo na Mh.Baba Askofu Dkt. Sollomon Jacob Massangwa.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.