Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Raymond Mwangwala ameanza ziara ya Siku ya Kwanza ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo na kusikiliza na kutatua kero za wananchi ndani ta Kata ya Pinyinyi.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Pinynyi Mhe.Mwangwala mesema serikali imeendelea kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo ambapo kwa kwts hiyo imetoa Milioni 580 za ujenzu wa shule mpya ya Sekondari Kata ya Pinyinyi , Milioni 20 za ujenzi wa darasa Moja shule ya msingi Pinyinyi na Milioni 89 za ujenzi wa Nyumba ya Daktari Zahanati ya Pinyinyi inayojengwa na TASAF
Aidha Mhe.Mwangwala amewapongeza wananchi kushiriki kuhakikisha miradi hiyo inakamilika "Nawapongeza wananchi wa kijiji cha Masusu kwa kujitoa kuchangia nguvu kazi katika mradi wa ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Pinyinyi kwa kutoa Shilingi Milioni 20 ikiwa hakika ni kuunga mkono Serikali ya Awamu ya sita ya Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassani" alisema Mhe Mwangwala
Baada ya kukamilika kwa ziara kwa siku ya kwanza Mhe Mwangwala ataendelea ziara katika Kata ya Sale.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.