ZIARA YA MKUU WILAYA YA NGORONGORO MHESHIMIWA RASHID MFAUME TAKA KATIKA KATA YA SAMUNGE TAREHE 09/10/2018.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Mfaume Taka amefanya ziara ya kawaida ya Siku moja ya kutembelea na kukagua miradi ya Maendeleo katika kata ya Samunge
Mh.Taka alianza kwa kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo cha afya Samunge ambapo mpaka sasa uchimbaji wa misingi ya nyumba 5 ambazo ni jengo la OPD,jengo la utawala , wodi ya Wazazi , Maabara, RCH, Nyumba ya watumishi six in one,imekamilika kwa Nguvu za Wananchi na serikali imechangia Shilingi milioni 400
Mh.Rashid Taka ametembelea ujenzi wa Nyumba ya waalimu six in one, Maabara Kemia na mabweni mawili katika Sekondari ya Samunge ambapo miradi yote hii inajengwa kwa nguvu za wananchi na Serikali
Wakati huo huo ametembelea ujenzi wa Chuo Cha Ufundi stadi VETA kinachojengwa na nguvu za wananchi kupitia Rika la Erumashari Samunge.Katika ujenzi huo amejionea majengo 8 yakiwa yanaendelea kujengwa ambapo majengo manne ambayo ni Jengo la utawala , Madarasa matatu na Karakana mbili yapo katika hatua ya lenta, madarasa mawili yamekamilika, na majengo mengine manne yapo katika hatua ya msingi,
Katika ziara Hiyo Mh.Kajurus Diwani WA Kata ya Samunge ameishukuru serikali ya awamu ya tano na Mh.Mbunge kwa kutoa Sh.M5 ya Mfuko WA Jimbo kwa Umaliziaji WA Jengo la Watumishi wa Zahanati ya Samunge.
Mh.Taka amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Samunge kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kujiletea Maendeleo yao wenyewe na kuunga mkono juhudi ya Serikali ya awamu ya Tano na amewahakikishia wananchi kwamba Serikali inatambua juhudi zao na itaendelea kuwaunga mkono kwa kuwaletea fedha za kumalizia miradi hiyo.
Mh.Taka alimalizia ziara yake kwa kuzungumza na mkutano mkubwa wa akina mama wa Kata ya Samunge ambapo walikusanyika katika eneo la Ujenzi wa Kituo cha Afya kwaajili ya kuweka taratibu za kuendelea kuchangia Ujenzi huo.
Mh.Rashid Taka akikagua msingi uliochimbwa kwa nguvu za wananchi wa ujenzi wa jengo la zahanati ya Samunge
Mh.Rashid Taka akipata maelezo kuhusu ujenzi wa nyumba ya mwalimu six in one katika Shule ya Sekondari Samunge
Mh.Kajurusi Dugo Diwani wa kata ya Samunge akieleza Jambo kwa Mh.Rashid Taka wakati akikagua jengo la nyumba ya waalimu Six in One katika sekondari ya Samunge.
Jengo la maabara ya Kemia likiwa katika hatua ya kumaliziaji katika shule ya Sekondari sambunge
Mh Rashid Taka alikagua pia majengo ya mabweni mawili katika sekondari ya Samunge yaliyopo katika hatua ya Lenta.
Pia Mh.Taka alikagua na kupata maelekezo ya ujenzi wa Chuo cha VETA samunge
Mh. DC alimaliza ziara yake kwa kuwasalimia wamama wa kata nzima ya samunge baada ya kumaliza kikao chao kwaajili ya kuchangia ujenzi wa zahanati ya Samunge
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.