Ngorongoro-, Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh. Rashid Mfaume Taka amewataka wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia hasa ukeketaji na ndoa za utotoni ili kufikia usawa wa kijinsia na kumpa fursa mwanamke kushiriki kikamilifu katika shughuli za kujiletea maendeleo
Mh. Taka ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yaliofanyika tar.8.3.2019 ambapo amewataka wanawake kubadirika kifikra kwani wao wenyewe ndio wanao tekeleza vitendo vya ukeketaji, pia amewataka wanaume wilayani hapa kuacha kuwaoza watoto wao katika umri mdogo ilikuwapa fursa ya kusoma na serikali haitafumbia macho vitendo kama hivyo.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ametoa rai kwa mashirika yasio ya kiserikali ambayo hayajishughulishi na kero na matatizo ya wananchi kuwa yatapotea huku akipongeza shirika la PALISEP na OXFAM kushirikiana na serikali kuiletea jamii maendeleo kwa kugawa mitamba na madume ya ng`ombe kwa vikundi vya wakinamama katika tarafa ya Loliondo.
Kwa upande wake Mkurugezi Mtendaji wa shirika la PALISEP Bw. Robert Kamakia amesema shirika lake limejizatiti kumwezesha mwanamke katika Wilaya ya Ngorongoro kujikwamua kiuchumi na kutambua haki zake za msingi ili kufikia usawa wa kijinsia.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kiwilaya yamefanyika katika kata ya Alaitole kijiji cha Esere yakiwa na kauli mbiu ya ‘chukua hatua kufikia usawa wa kijinsia kwa maendeleo endelevu’ambapo kwa mara ya kwanza kimataifa siku hii iliadhimishwa mwaka 1975 kutokana na vuguvugu la wanawake kudai haki zao kama ujira, kupunguziwa muda wa kazi na haki ya kupiga kura.
Imetolewa na Kitengo
Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Wanawake waliojitokeza kushiriki Maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika katika kijijicha Esere kata ya Alaitolei Wilaya ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.