Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe.Rashid Mfaume Taka amelitembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika katika banda hili siku ya tarehe 08/08/2020.
Akiwa katika banda hilo Mkuu wa Wilaya amejifunza pamoja na kujionea shughuli mbalimbali za Kilimo, Mifugo zinazofanyika katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ndani ya uwanja wa Themi -Njiro Arusha
Mhe. Taka amefurahishwa na bidhaa zinaoneshwa ndani ya banda la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro hasa katika utengenezwaji wa na Uchakataji wa Asali, utengenezwaji wa Tofali Pilipili utengenezwaji wa bidhaa za shanga zinazofanywa na Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali.
Ujumbe wa Nanenane mwaka 2020 ni : “Kwa maendeleo ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Chagua Viongozi Bora 2020”
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.