Afisa Maendeleo ya Jamii Bi.Flora Hindi amewataka watumishi wa serikali kufuatilia kwa ukaribu taarifa za hali ya hewa ili kujua mwenendo mzima wa mvua zinazotarajiwa kunyesha kwa wingi katika maeneo yetu.
Ameyasema hayo Leo tarehe 05 Octoba 2023 kwenye mafunzo kwa Watumishi juu ya taadhari ya mvua za EL NINO yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
"Taasisi inatakiwa kuchukua hatua za kuamisha wananchi wanao ishi katika mazingira hatarishi kama moniki, kuandaa fedha za tahadhari, vifaa maalumu vya uokoaji, kusafisha mito, mitaro na madaraja pia watu binafsi kuweka akiba ya chakula cha kutosha, na huduma zote muhimu wakati wote wa kipindi cha mvua" amesema
Pia Bi.Hindi amewataka wataalamu wa afya kuandaa madawa yakutosha ya magonjwa ya mlipuko kwani mvua hizi huwa na kawaida ya kusababisha magonjwa hayo na kusisitiza kuwa mtoa taarifa rasmi za majanga ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ambaye ni mkuu wa wilaya pekee yake.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.