Shirika la uhifadhi la FZS katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan limetoa Pikipiki moja itakayosaidia katika Shughuli za maendeleo kwa Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro hasa kwenye nyanda ya uhifadhi
Shirika la FZS limekabidhi pikipiki hiyo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ili kusaidia ufuatiliaji wa benki za uhifadhi za jamii (COCOBA) ambazo zinaiwezesha jamii kujipatia maendeleo kwa njia ya kuweka hisa, akiba na hatimaye kukopa mikopo isiyokua na riba.
Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Bw. Julius Fanuel -Technical Advisor kwa niaba ya Serengeti Ecosystem Program Manager na kumkabidhi Bw. Emmanuel Mhando kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Ikumbukwe kuwa mpaka sasa Shirika la FZS linafikisha idadi ya Pikipiki 12 ambazo wamezitoa na kuikabidhi Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.