• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhamira
    • Misingi mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utawala na Utumishi
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Vijana
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji na Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba za Vikao
    • Ratiba ya Mwenyekiti
    • Kata
      • Loliondo
        • Ololosokwan
        • Soitsambu
        • Enguserosambu
        • Maalon
        • Oloirien Magaiduru
        • Piyaya
        • Orgosorok
        • Oloipir
        • Arash
      • Ngorongoro
        • Alailelai
        • Naiyobi
        • Olbalbal
        • Nainokanoka
        • Kakesio
        • Ngorongoro
        • Eyasi
        • Endulen
        • Ngoile
        • Alaitolei
        • Misigyo
      • Sale
        • Sale
        • Malambo
        • Digodigo
        • Oldonyosambu
        • Samunge
        • Pinyinyi
        • Kirangi
        • Engaresero
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezw
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Majarida mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi

HALMASHAURI ZATAKIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUMOTISHA WAALIMU

Posted on: March 27th, 2019

HALMASHAURI ZATAKIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUMOTISHA WALIMU

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinaweka mikakati ya kuwamotisha walimu wapya wanaoripoti kazini kwa kuwafikisha katika vituo vyao vya kazi ikiwa ni pamoja na kuwalipa maslahi yao yote.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa sita wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya (REDEOA) na kusisitiza kuwa hatua hiyo iende sambamba na kuendelea kuwatembelea walimu hao katika vituo vyao vya kazi kuwasikiliza, kushauriana na kupatia ufumbuzi changamoto walizo nazo.

Amesema walimu hao wanaporipoti wanakuwa ni wageni katika wilaya hizo hivyo kuwaelekeza tu kuripoti katika shule walizopangwa haitoshi ni vyema kuweka utaratibu wa kutumia magari ya Halmashauri kuwafikisha walimu hao katika vituo vyao vipya vya kazi.

“Ninyi Maafisa Elimu hakikisheni walimu hao wanaporipoti wanalipwa maslahi yao ya msingi, lakini pia hamasisheni Halmashauri zenu kuwamotisha walimu kwa kuwapa vianzilishi vya maisha kama ambavyo Wilaya nyingine zinafanya. Wilaya za Mkoa wa Njombe tangu mwaka 2013 zimekuwa zikitoa motisha kwa walimu wapya wanaoripoti kwa kuwapa kitanda, godoro, gunia la mahindi, viazi na maharage, hii inamfanya mwalimu kujisikia yuko nyumbani, muige mfano huu,” aliongeza Waziri Mkuu Majaliwa.

Katika hatua nyingine Mhe. Majaliwa amewataka Maafisa Elimu hao kutumia mkutano huo kukumbushana wajibu wao katika kusimamia Elimu na kubadilishana uzoefu na mbinu mbalimbali za kusimamia elimu ili kuongeza ubora wa elimu hiyo.

“Mkutano huu umekuja kipindi muafaka kwa sababu matokeo ya upimaji wa Taifa wa ngazi mbalimbali yameshatoka, wote tunakumbuka upimaji umefanyika kwa mitihani ya darasa la nne, la saba, kidato cha nne na ile ya kidato cha sita, hii itoe fursa kwenu kujipima na kuona kama hatua mliyofikia ni nzuri na kama bado ni ya chini basi mbainishe changamoto zilizopelekea kuwa hivyo na kuweka mipango ya kuboresha,” alisema Mhe. Majaliwa

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amewataka Maafisa Elimu kusimamia Sera, Miongozo na Taratibu zinazosimamia utoaji wa elimu nchini huku akiwasihi maafisa hao kutoa taarifa zilizo sahihi kwani wakati mwingine taarifa zinazotolewa zinatofautiana na zile zinawasilishwa baada ya kufanyika kwa ukaguzi katika maeneo mnayoyasimamia

“Wakati mwingine mnatoa taarifa zisizo sahihi, kwa sababu kaguzi ambazo  zimekuwa zikifanyika zinaonesha kuna baadhi ya maeneo ambayo bado kuna mrundikano mkubwa wa wanafunzi kati ya 73 hadi 200 kwa upande wa sekondari na mazingira yanapokuwa katika hali hiyo si rahisi kutoa elimu bora, hivyo tutoe taarifa zilizo sahihi na taarifa hizi zikiwa sahihi itasaidia hata wakati wa uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza na kile cha tano,” aliongeza Waziri Ndalichako.

Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya Germana Mng’ao ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira ya kufundishia  na kujifunzia na kuahidi kufanya kazi kwa bidii katika nafasi yao ya kusimamia Elimu Tanzania.

Kauli mbiu ya mkutano huo ni “ELIMU BORA ITATUFIKISHA KATIKA UCHUMI WA KATI IFIKAPO 2025”.

Matangazo

  • TANGAZO LA RATIBA YA UCHAGUZI NA UANDIKISHAJI WA UCHAGUZI. September 26, 2024
  • TANGAZO LA UANDIKISHAJI VIJANA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA. October 01, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI.2. September 29, 2024
  • MATOKEO YA USILI WATENDAJI WA KIJIJI. September 29, 2024
  • Tazama zaidi

Habari Mpya

  • NGORONGORO MSTARI WA MBELE KUHIMIZA MATUMIZI YA NISHATI SAFI.

    May 09, 2025
  • KISIMA CHA MAJI SAFI KUCHIMBWA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA NGORONGORO

    April 25, 2025
  • ZIARA YA MWENYEKITI WA HALMASHAURI TARAFA YA NGORONGORO.

    April 28, 2025
  • WANAFUNZI 576 WA KIDATO CHA SITA KUFANYA MTIHANI WA TAIFA NGORONGORO.

    May 06, 2025
  • Tazama zaidi

Video

Afisa kilimo Ngorongoro aeleza na kufafanua namna ya kupata mazao yenye afya na mbegu bora kutumia katika kilimo.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Matokeo ya Upimaji darasa la Nne 2019
  • Taarifa na Matangazo
  • Mikataba na Miongozo
  • machapisho mbalimbali
  • Habari kwa umma
  • Taarifa kwa Umma
  • JINSI YA KUPATA SALARY SLIP
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO, VYUO VYA ELIMU YA KATI NA VYUO VYA UFUNDI JUNE 2019.
  • WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2023 NGORONGORO

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Rais
  • Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
  • NGORONGORO DC YOUTUBE CHANEL
  • MATOKEO YA UPIMAJI DARASA LA NNE 2019 WILAYA YA NGORONGORO

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.