Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kupitia Divisheni ya mifugo imeanza utekelezaji wa zoezi la upandikishaji ng'ombe kwa njia mrija kwa lengo la uboreshaji wa mifugo na kupata mbegu bora na zenye tija kwa wafugaji.
Uboreshaji wa mbegu za ng'ombe zinazotolewa ni ng'ombe wa maziwa pamoja na nyama ikiwemo mbegu ya boran, gylarando, simmental, fresian
Faida ya uboreshaji wa mbegu bora za ng'ombe ni kupata ndama bora kwa ajili ya ng'ombe bora, kuzuia kuenea kwa magonjwa ya mfumo wa kizazi kwa mifugo na njia rahisi ya kupata mbegu bora ya ndama inayopatikana kwa gharama nafuu.
Aidha, mbegu zinapatikana katika kituo cha Taifa cha uhimilishaji (NAIC) USA RIVER ARUSHA pamoja na URUS Company.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.