Loliondo ,Arusha.
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imezindua zoezi la kuwatambua na kuwapa vitambulisho wajasiriamali wadogo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli.
Akizungumza na mamia ya wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa kutoa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo hapo jana katika viwanja vya mnada wa Mji wa Wasso ,mwenyekiti wa Ulinzi na usalama wa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Mfaume Taka amezindua na kuwapatia wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo ishirini na mbili ambao walikidhi vigezo vya kupata vitambulisho hivyo.
Katika hotuba yake kwa wananchi Mh.Taka ametaja zoezi hilo kuwa ni kufuatia agizo la Raisi Dr.John Pombe Magufuli katika kikao chake na wakuu wa Mikoa na wilaya kote nchini pamoja na mawaziri mbalimbali ,Rais Magufuli alitoa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo 25,000 kwa kila Mkuu wa Mkoa na kuagiza kugawa kwa Halmashauri zote nchini ili kuwapatia wajasiriamali wadogo ambao mtaji wao hauzidi shilingi za kitanzania Milioni nne kwa mwaka.
Baada ya kutoa vitambulisho hivyo Mh.Taka ameeleza kuwa hakuna mamlaka yoyote itakayokuwa na idhini kudai ushuru au kodi yoyote kwa mjasiriamali aliyepewa kitambulisho hicho na kuongeza kuwa wataendelea kuwatambua na kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali watakaojiandikisha na kikidhi vigezo vinavyohitajika
Mh Taka ameeleza kuwa sifa za kupata kitambulisho hicho kuwa ni mjasiriamali au mfanyabishara lazima awe ni mtanzania,awe ni mjasiria mali ambae mauzo yake hayazidi milioni nne kwa mwaka,awe na kitambulisho kinachomtambulisha kimojawapo kati ya ,Leseni,kitambulisho cha kitaifa ,kitambulisho au barua kutoka kwa mtendaji wa kijiji,picha moja ya passport.Baada ya kuwa na viambatanisho hivyo Mkusika atajaza fomu na kulipa shilingi elfu ishirini na kupatiwa kitambulisho chake.Ameeleza pia kuwa zoezi hilo litaendelea likiendeshwa na timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na ofisi za TRA Ngorongoro katika minada yote kulingana na Ratiba na siku ya minada katika maeneo yote Wilayani Ngorongoro
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mh.Rashid M.Taka akizindua zoezi la kuwapatia wajasiriamali wadogo vitambulisho katika viwanja vya mnada mji wa Wasso
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.