Ngorongoro Arusha ,
Kamati hiyo ya ALAT Mkoa wa Arusha ikiongozana na na wajumbe ilinza kutembelea mradi wa maji wa Mji wa Loliondo ,mradi wa rea,mradi wa barabara Wasso-Sale , Kituo cha Afya Sakala na kuhitimisha katika kata ya Samunge kwa kukagua mradi wa Chuo cha Veta na kituo cha Afya
Wajumbe walitembelea kituo cha afya Sakala ambapo Kaimu Mganga Mkuu (W) aliwasilisha taarifa kwa wajumbe ikionesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ilipokea kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mia nne (400,000,000) tarehe 16/01/2018 kutoka Serikali Kuu kwa hisani wa Ubalozi wa Canada chini ya mfuko wa pamoja wa Afya kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Kituo cha Afya Sakala.Majengo manne yamejengwa ambayo ni jengo la upasuaji, jengo la kuhifadhia maiti, wodi ya wazazi pamoja na nyumba ya mtumishi.Hadi sasa Mradi umegharimu jumla ya tshs 433,000,000 ikiwa Tshs 33,000,000.00 ni mchango wa Halmashauri. ujenzi unaendelea na unategemea kumalizika ifikapo mwezi Januari 2019.
Wajumbe wa ALAT walipata nafasi ya kusikiliza taarifa ya Meneja wa Mamlaka ya Maji Mji wa Loliondo ikionesha Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji, inatekeleza mradi wa majisafi ndani ya Mji wa Loliondo. Wizara imekasimu utekelezaji wa mradi huu kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira jiji la Arusha (AUWSA) kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mji wa Loliondo (LOLUWSA). Mradi huu ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa kwa kutumia fedha za ndani kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Kazi zinazotarajiwa kufanyika katika mradi huu ni kama ifuatavyo;
Gharama za mradi huu kwa mujibu wa mkataba ni kiasi cha Tshs. 366,082,956.33/- na Mkandarasi anayejenga mradi huu ni kampuni ya Kitibu Company Limited.
Wajumbe walipata taarifa ya Ujenzi wa Barabara ya lami ya LOLIONDO -MTO WA MBU ikieleza kuwa Mradi unatekelezwa kwa km 49 kuanzia Wasso hadi Sale, mradi ulianza tarehe 18/10/2017 na unategemewa kukamilika tarehe 17/10/2019. Gharama ya mradi mzima kwa km 49 ni Tshs. 87,126,445,712.35 ikiwa ni pamoja na VAT. Mkandarasi wa Mradi huo ni CHINA WU YI CO.LTD na ametekeleza mradi kwa asilimia 24.85%.
Vile vile wajumbe walipata nafasi ya kutembelea mradi ya usambazaji umeme vijijini REA .Kaimu Meneja TANESCO (W) aliwaeleza wajumbe kuwa Usambazaji wa umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa kwanza katika wilaya ya Ngorongoro umezinduliwa rasmi tarehe 19/08/2017 katika kata ya Digodigo na mkandarasi anayetekeleza mradi huu ni NIPO GROUP LTD.Mkandarasi alianza rasmi kutekeleza mradi huu katika Wilaya ya Ngorongoro tarehe 01/06/2018 na maeneo yanayopitiwa na mradi ni 37.Umbali wa laini za umeme utakuwa km 182 kwa msongo mkubwa wa kilovoti 11 na km 72.3 kwa msongo mdogo wa kilovoti 0.4 (400V). Hadi sasa msongo mkubwa wamevuta waya umbali wa km 14 na msongo mdogo umbali wa km 0.7, mashimo yamechimbwa km 07 kuelekea Magaiduru.
Wajumbe wa ALAT pia walipata nafasi ya kutembele Mradi wa nyumba ya waalimu 6.1 uliofadhiliwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na ulitegemea kugharimu kiasi cha Tshs 141,000,000 hadi kukamilika kwake. Hadi sasa Mradi umekamilika na umegharimu jumla ya tshs 127,988,464 tu hivyo kuwa na Bakaa ya Tshs 13,011,536.Vile vile maabara ya Kemia katika shule ya sekondari Samunge ambayo imejengwa kwa fedha za EP4R na ulitengewa kiasi cha Tshs. 30,000,000 na kiasi kilichotumika ni 27,000,000 ambazo zilitumika kumalizia ujenzi pamoja na kuweka vifaa katika maabara hiyo.
Katika kata ya samunge wajumbe wa ALAT walitembeelea Mradi wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Samunge ambao ulianza kutekelezwa kwa nguvu za wanawake wa Samunge kwa kuchangisha fedha kiasi cha Tshs. 10,000 kwa kila mmoja na kuweza kujenga jengo mpaka hatua ya Lenta.Aidha Mhe. Mbunge William ole Nasha alisaidia kwa kupaua jengo hilo na Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ilitoa kiasi cha Tshs. 20,000,000 kwa ajili ya umaliziaji ambapo kwa sasa mradi upo katika hatua ya umaliziaji.
Baada ya ziara hiyo Mheshimiwa Mwenyekiti aliwashukuru wajumbe waliotembelea miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongroro na kutoa pongezi nyingi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa utekelezaji na usimamizi mzuri wa miradi hiyo kwani thamani ya fedha imeonekana.Aidha alitumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro kwa kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo yao na kuwaasa Halmashauri nyingine kuiga mfano wa wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro. Katika kuunga mkono juhudi za akina mama wa Samunge wajumbe wa ALAT walichangia walichangia kiasi cha Tshs 220,000/-
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Bw.Peter Juma wateta jambo na Mkamu mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Arusha Mh. ...wakati walipotembelea mradi wa Barabara ya lami inayojengwa kutoka WAASO -SALE
Wajumbe wa ALAT mkoa wa Arusha wakipata maelezo kutoka kwa Diwani wa kata ya Samunge baada ya kutembelea ujenzi wa chuo cha VETA
Wajumbe wa ALAT wakipata maelezo ya Mradi wa usambazaji wa Mji katika Mji wa LOLIONDO
.Pichani ni wajumbe wa ALAT mkoa wa Arusha walipotembelea Ofisi za TANESCO wilaya ya Ngorongoro kupata taarifa ya Utekelezaji wa Usambazaji wa Umeme vijijini (REA)
Wajumbe wa ALAT mkoa wa ARUSHA walipotembelea nyumba ya watumishi katika zahanati ya Samunge na walipaata nafasi ya kuwaunga mkono wakinamama hao kwa kuwachangia kiasi cha shilingi 220,000
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.