Na Gabriel E.Mpeho
Kamati ya Fedha Ungozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Emanuel Tonge ,waheshimiwa Madiwani na wakuu wa Idara na vitengo leo tarehe 07 Novemba 2023 imeendelea na ziara yake ya ukaguzi miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya Ngorongoro kwa siku ya pili ambapo ukaguzi wa miradi ni moja ya jukumu la Kamati hiyo.
Kamati imempongeza Mkurugenzi Mtendaji Bw.Nassoro Shemzigwa kwa usimamizi mzuri kwa miradi inayoendelea ndani ya Wilaya ya Ngorongoro pamoja na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayoonekana kwani miradi hiyo inakwenda kuwanufaisha wananchi moja kwa moja.
Kamati imetembelea miradi ya maendeleo katika Chuo cha Ualimu cha Ngorongoro, Shule ya msingi Losirwa, Kukagua Vifaa tiba kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro, kisha kukagua jengo la utawala la Halmashauri Wilaya ya Ngorongoro.Aidha kamati ya Fedha Uongozi na Mipango imekagua kukagua vifaa tiba vya kisasa vilivyoletwa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo X-ray ya Meno yenye thamani ya Shilingi MILIONI 48,Jenereta kiasi cha Shilingi Milioni 63,Digital X RAY Shilingi milioni 295,Mashine ya Kufulia Shilingi milioni 10 na kufanya jumla ya zaidi ya Shilingi 992.
Aidha Kamati ya fedha licha ya kuridhishwa na maendeleo mazuri ya ujenzi katika jengo la utawala, imewataka wahandisi kuongeza kasi na ujenzi ili kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda uliyowekwa.
Akiongelea mradi wa shule ya Msingi Losirwa, Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Emmanuel Tonge
ametoa pongezi kwa wasimamizi wa mradi huo akiwemo mkuu wa shule ya msingi ya kirtalo Amani Olotu wenyeviti wa vitongoji (Bw. Kasino Moiyoi, Kitongoji cha Losirwa na Bw. Danika Letura, kitongoji cha Empopong'i) pamoja na Mwenyeti wa kamati ya ujenzi kwa kazi kubwa waliyoifanya na wanayoendelea kuifanya.
"Kwa niaba ya Kamati ya Uongozi na Mipango kwenye bajeti ya Halmashauri tutaleta milioni ishirini kwaajili ya kuongeza nguvu ya Ujenzi wa Shule mpya ya Losirwa ili iweze kuanza maramoja kutapisha Shule ya msingi Kirtalo" amesema Mhe Tonge
Naye Mwenyekiti wa Kitongoji cha Losirwa Mhe.Danika Letura amesema kabla ya shule hii watoto walitembea kilomita 4 kufika shule, wanyama wakali njiani ilikua nichangamoto hali iliyokuwa inatishia usalama wa watoto
Hata hivyo Wananchi wametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kwa fedha za miradi ya maendeleo.
Aidha Kaiumu Afisa Elimu Msingi Wilaya Ndugu Joachim Mgonja ameeleza kuwa Shule ya msingi Losirwa imegharimu shilingi milion 638 kupitia Fedha kutoka Serikali kuu kupitia Mradi BOOST na Utekelezaji mradi umefika Asilimia 95% ya Ujenzi
Aidha Kamati imetumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za kutekeleza miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Ikumbukwe Kamati ya mipango na fedha inajukumu la kukagua miradi inayoendelea ndani ya Wilaya ya Ngorongoro.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.