Kamati ya fedha, uongozi na mipango Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imefanya ziara ya kuyembelea miradi ya maendeleo Tarafa ya Ngorongoro ambapo wametembelea shule ya sekondari ya Ngorongoro girls kukagua maendeleo ya ukarabati wa matundu ya vyoo, huduma ya maji na kuridhishwa namna shughuli zinavyoendelea, ukarabati wa mabweni shule ya msingi Endulen, ukarabati wa madarasa tisa shule ya msingi Ndiao, shule ya msingi Kakesio ukarabati wa matundu ya vyoo sita, pamoja na ukarabati wa nyumba ya walimu.
Ziara hiyo imeanza leo tarehe 5 Februari na kutarajia kumalizika siku ya ijumaa ya tarehe 7 Februari 2025 kwa kutembelea kata zote zilizopo Tarafa ya Ngorongoro.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.