Kaimu Mganga Mkuu Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro Dr. Libori Tarimo akiwa kwenye kikao na kamati ya uendeshaji wa shughuli za Afya wilayani Ngorongoro katika Kituo Cha Afya Loliondo kusikiliza na kutatua kero za Watumishi.
Lengo la kufanya kikao hicho ni kudumisha uhusiano mzuri baina ya Watumishi na Uongozi wa Halmashauri ili kuchochea utoaji bora wa huduma za kiafya kwa Wananchi.
Katika kikao hicho Dkt. Libori amewasisitiza Wahudumu wa afya kufanya kazi kwa weledi, ushirikiano, kuwa na uwelewano mzuri kazini pamoja na kuzingatia maadili bora ya kitabibu.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.