Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Bw.Raphael J.Siumbu, anawatangazia wananchi wote, kushiriki maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yatakayofanyika tarehe 16.06.2019, kwenye viwanja vya shule ya Msingi Nainokanoka , kuanzia saa 02:30 asubuhi.
Maadhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali zitakazofanywa na watoto wenyewe, ikiwemo maandamano yatakayoongozwa na Mgeni Rasmi, pamoja na burudani zilizobeba jumbe mbalimbali zinazohusu Haki, Wajibu na Maendeleo ya Mtoto wa Afrika.
Mgeni rasmi atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Mfaume Taka
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.