Maafisa Elimu Kata kutoka kata 28 ndani ya Wilaya Ngororongoro wapatiwa mafunzo ya udereva pikipiki.Mafunzo hayo yamefunguliwa leo rasmi na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro Bw.Victor Kaiza na yataendeshwa kwa kwa muda wa sikutatu.Kwa niaba ya mkurugenzi Bw.Victor Kaiza Amewasihi na Maafisa Elimu kata kushiriki vyema katika Mafunzo hayo ya kuwajengea uwezo wa kutumia Vyombo vya Moto(PIKIPIKI)na kuishukuru serikali ya awamu ya Tano kwa Msaada huo Mkubwa wa Usafiri wa Pikipiki utakaowawezesha Maafisa hao kutembelea Shule kukagua na kuinua ubora wa Elimu katika Wilaya ya Ngorongoro.Hata hivyo Neema hiyo imekuja baada ya siku chache serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi kukabidhi pikipiki 2894 kwa Waratibu wa Elimu kwa ngazi ya kata kote nchini
Afisa Elimu Msingi (W)Ngorongoro Ndugu Tumsifu Mushi akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi Bw.Kaiza katika mafunzo ya Udereva kwa Maafisa Elimu Kata 28 za Wilaya ya Ngorongoro.
Kaimu Mkurugenzi (W)Ngorongoro Ndugu Victor Kaiza akifungua mafunzo ya Udereva kwa Maafisa Elimu Kata 28 za Wilaya ya Ngorongoro katika ukumbi wa Shule ya Msingi Wasso
Mkufunzi Michael Richard akitoa maelekezo wakati wa Mfunzo
Pikipiki 28 zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi Teknolojia na Ufundi zimewasili Loliondo yalipo makao makuu ya wilaya ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.