Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mhe. Kanali Wilson Sakulo alitoa maelekezo kwa mganga mkuu wa Wilaya ya kupeleka wahudumu wa afya na kutoa matibu ya haraka ili kukomesha ugonjwa wa kuhara uliowakumba Wananchi Kata ya pinyinyi.
Mheshiwa Sakulo alitoa maelekezo hayo alipotembelea Kata hiyo Kutoa elimu ya mpiga kura mnamo tarehe 26 Septemba 2024 na kupokea kero kutoka kwa wananchi wa Pinyinyi juu ya ugonjwa wa kuhara ambao umewasumbua kwa kipindi hiki cha kiangazi.
Timu ya wahudumu wa afya wamefika na kuanza utekelezaji wa maelekezo hayo kwa kujali afya za Wananchi wa Kata hiyo katika Kijiji cha Ndikinya ili kuukabili ugonjwa huo.
Aidha timu hiyo kwa usimamizi wa Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Libori Tarimo imetoa Elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na vyoo, kuvaa buti maalumu wakati wa Kilimo, kuchemsha maji na Kuacha mazoea ya kuoga mtoni ili kujinga na changamoto ya ugonjwa huo wa kuhara pamoja na magonjwa mengine.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.