Ngorongoro ,Arusha
2 Nov. 2018
Makatibu wakuu wa Wizara sita tofauti wametembelea baraza la wafugaji Ngorongoro Wilayani hapa kuzungumza nao ili kutatua kero zao.Ziara hiyo imejiri hapo jana 1 Disemba 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kufuati ahadi ya katibu mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Olegabrel siku chache zilizopita alipotembelea baraza hilo, ambapo aliahidi wanachi hao kuwa ili kutatua changamoto zao ni lazima akutane na makatibu wenzake wa wizara husika ili kujadili kwa pamoja namna ya kutatua kero za wanachi.
Hata hivyo makatibu sita wa Wizara tofauti ikiwemo Pro.Adolf Mkenda Katibu Mkuu Maliasili na Utalii, Prof.Kitila Mkumbo Katibu Mkuu Wizara ya Maji na umwagiliaji ,Prof Elisante Ole Gabriel Katibu mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Doroth Mwanyika Katibu Mkuu Wizara yaArdhi nyumba na maendeleo ya makazi ,Dr Jim Yonaz Naibu katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano na Joseph Mwalongo Katibu mkuu Ofisi ya Mkamu wa Raisi Muungano na Mazingira wamebainisha kuwa wamesikiliza kero za wananchi hao na kuongeza kuwa watakutana kujadili namna sahihi ya kutatua changamoto zilizobainishwa bila kuathiri upande wowote.
Kikao kiliudhuriwa pia na Ndugu Raphael Siumbu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Afisa Mifugo na Uvuvu (W)Ngorongoro Bw.Chobi Chubwa na upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro Mh.Methew Siloma na Diwani wa kata ya Arash kwa niaba ya uongozi wa Wilayani ya Ngorongoro amewashukuru makatibu hao kwa kutembelea baraza la wafugaji na kutaja kuwa wanaamini ujio wa viongozi wa wizara hizo itasaidia kutatua kero zilizopo katika eneo hilo la tarafa ya Ngorongoro.
Imetolewa na
Kitengo cha habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mhifadhi Mkuu wa Mmalaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dr.Manongi akisalimiana na katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na uvuvi Prof.Elisante Olegabriel wakati wa ziara ya makatibu wakuu 6 wa wizara tofauti tofauti
Prof Olegabriel Katibu Mkuu wizara ya Mifugo na Uvuvi akivishwa zawadi ya asili ya Kimasai
Dr Jim Yonaz Naibu katibu mkuu Wizara ya Mawasiliano akivishwa zawadi ya asili ya Kimasai
Prof Kitila Mkumbo Katibu Mkuu wizara ya maji na umwagiliaji akivishwa zawadi ya asili ya Kimasai
Picha ya Pamoja kati ya Mkatibu wa kuu sita na viongozi wa baraza la wafugaji baada ya kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.