Mh.Rashid Taka-Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro akimkaribisha Mh.Mrisho Gambo-Mkuu wa mkoa wa Arusha katika zoezi la kupokea Mwenge wa Uhuru wilaya ya Ngorongoro
Mh.Siloma -Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro akimkaribiisha Mh.Mrisho Gambo Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwenye zoezi la kuupokea Mwenge wa Uhuru katika Eneo la Olduvai
Mhe. Kiongozi Wa Mbio Za Mwenge Wa Uhuru Kitaifa, Charles Fransis Kabeho akizindua barabara yenye urefu wa kilomita kumi na nne (14) kutoka katika Lango la Lemala kupitia Kijiji cha Irkeepus hadi kijiji cha Nainokanoka kata ya Nainokanoka, ni kati ya sehemu ya barabara yenye urefu wa kilomita sabini na nane (78kms ) za barabara kuu kutoka View Point,kupitia kata ya Nainokanoka ,kata ya Alailelai na kuishia kata ya Naiyobi.
Ndugu Charles Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, amezindua Ujenzi wa nyumba ya watumishi (2 in 1) ambao ulianza rasmi mwaka 2013 na kukamilika mwezi Juni 2016. Kila nyumba moja ina vyumba vitatu (3) vya kulala, sebule, choo, bafu, stoo na jiko. Ujenzi huu umefadhiliwa na taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) ambao hadi kukamilika umegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania 107,852,524/=
Ndugu Charles Kabeho Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, amezindua Mradi wa huduma za ugani, Udhibiti wa magonjwa ya mifugo ambao umelenga kutatua changamoto za magonjwa ya mifugo, yanayoambukiza binadamu, wanyamapori na mifugo, kuzijengea uwezo kamati za usimamizi wa majosho, kutoa chanjo za mifugo aina ya Homa ya mapafu ya ng’ombe, Sotoka ya Wanyama Wadogo (Mbuzi na Kondoo) na kutoa chanjo ya kimeta.
Ndugu Charles Francis Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa amezindua Miradi ya Ujenzi wa majengo unahusisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kidato cha tano na sita lenye kuchukua wanafunzi 80, ujenzi wa matundu 10 ya choo pamoja na ukarabati wa maabara ambapo umegharimu Tsh. 178,963,640.00/= hadi kukamilika katika shule ya Sekondari Nainokanoka.
Ndugu Charles Francis Kabeho kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa akipewa zawadi katika boma la Seneto baada ya kutembelea kujionea shughuli za kiuchumi wanazofanya
Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ,viongozi wa Dini na viongozi wa kisiasa wakilisikiliza Risala ya Utii iliyosomwa na katibu tawala wa wilaya mbele ya Kiongozi wa Mwenge wa uhuru Taifa Ndugu Charles Kabeho
Vikundi Vya burudani vikitumbuiza eneo la mkesha wa Mwenge wa Uhuru
Mh.Diwani wa Kata ya Ninokanoka akiwakaribisha wageni wa Mwenge wa Uhuru
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.