Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo katika kuboresha miundombinu ya usafiri kwa kutoa zaidi ya Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa daraja linalounganisha Kijiji cha Oldonyosambu na Kijiji cha Jema.
Ujenzi wa daraja hilo unaendelea kwa kasi, ikiwa ni juhudi za kuhakikisha mawasiliano kati ya vijiji hivi viwili yanaimarika, hatua inayotarajiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa maeneo hayo.
Awali, Mto Mmbaga ulikuwa changamoto kubwa kwa wananchi, hasa wakati wa msimu wa mvua ambapo mawasiliano yalikatika kabisa. Kukamilika kwa daraja hili kutamaliza kero hiyo na kufungua fursa zaidi za maendeleo kwa jamii.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.