Mhe. Emmanuel Oleshangai Mbunge Jimbo la Ngorongoro leo tarehe 18 Januari 2024 amewakilishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Ngorongoro Mh Mohamed Bayo(Diwani) pamoja na Katibu wa Ccm wilaya Bw. Abubakar Ghati katika zoezi la kuwapa pole wanafunzi na Uongozi wa Shule ya Sekondari Loliondo kufuatia kuunguwa kwa bweni Wiki iliyopita.
Sambamba na Pole za Mh Mbunge Pia amekabidhi magodoro 20 na shuka za vitanda kwaajili ya wanafunzi waliopoteza Mahitaji yao muhimu kufuatia ajali hiyo.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.