Mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya ya Ngorongoro(Diwani) Mhe Mohamed Bayo leo tarehe 03 Octoba 2023 amefanya kikao na chenye lengo la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wanaojiandaa kujiunga na elimu ya sekondari kidato cha Kwanza 2024 na kuwata wahusika kuboresha mfuko wa Kusaidia watoto mpaka kufikia idadi ya watoto 200 kwa Kuongeza maboresho ya uchangiaji waweze kutoa msaada mpaka kuwafikia watoto wote wenye uhitaji wilaya nzima.
Pia watendaji wengine wa serikali pamoja na viongozi wa dini wameipongeza serikali na Mhe.Bayo kuwa mstari wa mbele katika kujitoa na kuamua kuisaidia jamii kupitia mfuko wa maendeleo ili kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata haki yao ya kielimu ili kuleta maendeleo kwenye jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe.Bayo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Orgosorock amewaomba wazazi kuwasisitiza watoto wao wasome kwa bidii na kuzitaka shule zisizo za serikali kutoa ushirikiano na msaada pale panapobidi ili kuwasaidia watoto katika wilaya ya Ngorongoro.
Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi Halmashauri kikiudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa vitongoji, walimu wakuu, viongozi wa mfuko wa maendeleo wa kata pamoja watendaji wa kata
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.