Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Murtallah Sadiki Mbillu ameanza utekelezaji wa maagizo ya waziri wa Tamisemi Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyoyatoa kuhusu kuwajengea mlMaafisa usafirishanji vituo (Bodaboda) kwaajili ya kuwawekea mazingira bora ya kufanyia kazi.
Akizungumza na Maafisa wasafirishaji hao katika moja ya kituo Cha bodaboda wilayani hapo Mkururugenzi amesema utekelezaji huo umekuja baada ya Waziri wa TAMISEMI kutoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini, kuwajengea maafisa hao wa usafirishaji vituo vya kuegesha vyombo vyao vya moto.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mohamed Bayo amewataka vijana hao kujiunga na Vikundi ili kunufaika na Mikopo ya Asilimia 10 ya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu inayotolewa na Halmashauri kwa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Bayo amesema kuwa Maafisa usafirishaji hao wajiunge katika vikundi na kutambuana ili kuweza kufahamiana na kutoa huduma bora kwa Wananchi na kupunguza malalamiko ya wateja wanaopata madhara ya kuangushwa ama kuibiwa wakati wanatumia usafiri huo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya ngorongoro Bw. Daniel Bura amewasihi Maafisa wa usafirishaji hao kujiunga kwenye vikundi ili waweze kutambulika kwa sifa waweze kupata mikopo hiyo inayotelewa na Halmashauri kwa urahisi zaidi.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Wasso kaskazini Ndg. Lagwe Pemba kwa niaba ya Wananchi ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya awamu ya sita pamoja na uongozi wake ukiwemo uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa kazi unaoendelea kuifanya.
"Tunamshukuru Mhe.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutengeneza mazingira bora ya kufanyia kazi kwa wakazi wa Mamlaka ya mji mdogo wa Loliondo, hii imetuonesha jinsi gani serikali yetu inavyotujali, amesema Ndg. Pemba
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.