MKUU wa Wilaya ya Ngorongoro, Raymond Mwangwala, amesema kuwa Halmshauri ya Wilaya ya Ngorongoro, kwakushirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, imeanza uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi utakaodumu kwa zaidi ya miaka 20
Mpango huo wa matumizi ya ardhi wa halmashauri hiyo, utatoa taswira sahihi ya matumizi ya ardhi, ikiwemo malisho, kufanya ufuatiliaji wa mabadiliko ya matumizi ya ardhi na kubaini athari zake kiuchumi pamoja na mabadaliko ya tabianchi.
Dc Mangwallah alitoa rai hiyo leo wilayani Ngorongoro, wakati akifungua kikao cha uandaaji wa mpango wa matumizi ya ardhi wa halmashauri ya wilaya hiyo na kusisitiza wadau walioshiriki mkutano huo kutoa maoni yao, ili ardhi hiyo iweze kupangwa vema.
Amesema mpango huo utasaidia watumiaji mbalimbali wa ardhi, kutambua ukubwa,ikiwemo vijiji kujikwamua kiuchumi kwa kuanisha maeneo muhimu kwa ajili ya uchumi kukua.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.