Mkuu wa mkoa wa Arusha mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo tarehe 21/06/2018 amehudhuria baraza maalum la hoja za mkaguzi mkuu wa serekali katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Mkuu wa mkoa baada ya kusikiliza hoja katika baraza maalum la hoja alipata muda wa kuhutubia madiwani, watumishi na wananchi wachache waliohudhuria.
Aliwataarifu madiwani kuwa tumepata shilingi billioni moja na millioni mia tano fedha za kitanzania kwa ajili ya kujenga hospitali ya wilaya hivyo wakae na kupendekeza eneo la kujenga hospitali hiyo. Alieleza pia kuwa wadau wengine kama mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wameahidi kutoa bilioni moja ambapo wilaya ya Ngorongoro itapata millioni mia tano na milioni miatano zitakazobakia zitapelekwa karatu kusaidia ujenzi wa hospitali ya wilaya pia.
Mkuu wa mkoa alieleza umuhimu wa kuwa na hospitali ya wilaya kuwa itapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali za rufaa hasa Mount Meru kwani wagonjwa wengi watatibiwa katika ngazi za hospitali za wilaya.
Aidha baraza la madiwani wamejadili na kuamua kuwa hospitali ya wilaya ijengwe Sakala.
Kuhusu baraza la wafugaji, Mkuu wa mkoa aliwaeleza waheshimiwa madiwani kuwa serikali haina mpango wa kufuta baraza la wafugaji ila inachofanya ni kupeleka halmashauri fedha za miradi ya maendeleo za baraza ili zigawanywe kwa pamoja kwa maendeleo ya Ngorongoro hivyo wanaopotosha ukweli waache kudanganya wananchi
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.