NGORONGORO ,ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo amezindua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ngorongoro katika kijiji cha Maaloni kata ya Oloirien Magaiduru na kuitaka Uongozi wa Halmashauri kukutana mapema na wananchi ili kukamilisha taratibu za kuanza kwa ujenzi huo.
Gambo amezindua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwa mara ya kwanza juzi tarehe 13. 1. 2019 wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kikazi wilaya hapa ambapo amemuagiza mkuu wa Wilaya Mh. Rashid Mfaume Taka kukutana na wananchi ambao maeneo yao yatamegwa na ujenzi wa Hospitali ili watafutiwe maeneo ya fidia.
Wakizungumza na Mkuu wa Mkoa baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Maaloni wamemueleza mkuu wa mkuoa furaha yao kwa Hospitali ya Wilaya kuhamia katika kijiji chao lakini wakatoa ombi la kulipwa fidia ya mashamba yao walizodai kuwa tayari wameshalima ambapo Gambo ameelekeza Halmashauri kutathmini gharama zilizotumika pamoja na kuzungumza na uongozi wa kijiji ili kuwafidia wananchi hao
Kwa Upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi - CCM Mkoa wa Arusha Mussa Matoroka ametoa Rai kwa wote waliopewa ridhaa ya kujenga Hospitali hiyo waanze kazi mara moja na kwa uaminifu.
Wakati hayo yakijiri tarafa ya Loliondo Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni Mbunge wa Wilaya ya Ngorongoro Mh. Williama Tate Olenasha akiwa miongoni mwa Viongozi walioambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo tarehe 13.01.2019 amezindua shule mpya ya Msingi Indoinyo katika kata ya Olaitolei tarafa ya Ngorongoro na kubainisha kuwa shule hiyo inafanya idadi ya shule za msingi zilizosajiliwa na serkali kwa miaka 2 wilayani hapa kuwa 9 na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na serikali ya Awamu ya Tano ili kumuunga mkono jitihada za Mh. Rais John Pombe Magufuli katika kuboresha miundo mbinu ya Elimu
Mh. Olenasha ametoa Rai kwa wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro kutumia kipindi cha utawala wa Rais magufuli kama fursa ya kujikwamua kufikia maendeleo haswa Elimu ambayo serikali inatoa bure na kuongeza hakuna sababu ya Mzazi au mlezi kushindwa kumpeleka mtoto shule.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.