Katika siku ya pili ya ziara yake tarehe 23/06/2018 Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo alitembelea katika mradi wa Veta Samunge unaojengwa na rika la Erumashari. Baada ya kukagua mradi huo mkuu wa mkoa aliwapongeza wananchi kwa kujitolea kwa hali na mali katika shughuli za maendeleo na aliahidi kuchangia shilingi milioni mbili (2,000,000) fedha za Kitanzania. Naye mwenyekiti wa halmashauri mheshimiwa Mathew Siloma alichangia shilingi laki nne kwa ajili ya kununulia mifuko ishirini ya sementi.
Pia mkuu wa mkoa ameahidi shilingi milioni mia nne kwa ajili ya upanuzi wa zahanati ya samunge. Hii imekuja baada ya wananchi kumweleza mkuu wa mkoa kuwa watu wa samunge hasa wakinamama wajawazito wanapata shida kufuata huduma za afya wasso. Baada ahadi hiyo wananchi wa samunge walimuahidi mkuu wa mkoa kuwa na wao watakusanya mawe, mchanga , kokoto na kuchimba msingi ili fedha hiyo ifanye kazi kubwa.
Mkuu wa mkoa pia alitembelea na kukagua ujenzi wa bwalo, nyumba ya walimu na bweni la wasichana unaoendelea katika shule ya sekondari digodigo, umaliziaji wa jengo la kituo cha afya mugholo na baadaye kuhutubia wananchi katika kijiji cha Digodigo.
Kuhusu umeme wananchi wameahidiwa kuwa kufikia mwezi wa tisa umeme utakuwa umeshafika maeneo ya Samunge na Digodigo hivyo waanze kuandaa nyumba zao kwa ajili ya kufungiwa umeme.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.