Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Kanali Wilson Sakulo, amewatembelea majeruhi wa ajali ya lori aina ya Fuso iliyotokea jana tarehe 10 Novemba 2024, katika eneo la Zero Zero - Wasso. Ajali hiyo ya lori lililokuwa limebeba vijana wanamichezo waliokuwa wanatoka kijiji cha Soitisambu wakirejea baada ya kushiriki katika michezo. Ajali hiyo imesababisha majeruhi 33, ambao wote wamefikishwa Hospitali ya Wasso kwa ajili ya matibabu.
Mhe. Sakulo amewapa pole majeruhi hao pamoja na familia zao, huku akiwatakia uponaji wa haraka. Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya ametumia fursa hiyo kutoa tahadhari kwa madereva, akiwataka kuwa makini wanapoendesha vyombo vya moto ili kuepusha ajali zinazopeleka madhara makubwa kwa jamii.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.