Loliondo-Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, mheshimiwa Rashid Taka , amewataka Maafisa Watendaji wa Kata na vijiji, wilayani Ngorongoro kulipa umuhimu zoezi la ugawaji vitambulisho vya wajasiriamali, alipokutana nao kwenye ukumbi wa mikutano, halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mkuu huyo wa Wilaya , ametoa wito huo alipokutana na watendaji hao wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro na na kuwakabidhi jumla ya vitambulisho elfu sita 6000 Kupitia Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro , na kuwataka , kuhakikisha wajasiriamali wote katika maeneo yao wamepata vitambulisho hivyo.
Muheshimiwa Taka ametoa ufafanuzi, juu ya umuhimi wa zoezi hilo na kusema kuwa, lengo la serikali ni kutambua idadi ya wajasiriamali walio katika sekta isiyo rasmi, kutokana na ukweli kuwa, wafanya biashara wengi wanakwepa kulipa kodi huku wafanya biashara wachache wakibeba mzigo wa kulipa kodi kila mwaka.
Kupitia vitambulisho hivyo, kutawezesha kutambulika kwa wajasiriamali walio katika sekta isiyo rasmi, kuweza kuwasimamia wajasiriamali hao kukua kwa kukuza mitaji ili na kuwawezesha kufikia ngazi ya wafanyabiashara.
Licha ya kuwa serikali imeweka mkakati wa kulitambua kundi hilo la wajasiriamali kwa kuwapa vitambulisho, lakini kumekuwa na upotoshaji juu ya vitambulisho hivyo, unaosababisha jamii kutokuelewa lengo la serikali la kugawa vutambulisho hivyo, na kushindwa kupima ni yupi mfanyabiashara na yupi ni mjasiriamali.
Hata hivyo Muheshimiwa Taka amewata watendaji hao, kuhakikisha wajasiriamali wote katika maeneo yao, wanapatiwa vitambulisho ili kila mjasiriamali aweze kutambulika na kuweza kufanyabiashara yake kihalali bila kubughudhiwa.
"Pia amewataka watendaji hao kutoweka masharti magumu ya upatikanaji wa vitambulisho hivyo kutokana na jografia ya maeneo yao ili wafanyabiashara wadoogowadogo waweze kuvipata kwa Urahisi.
Imetolewa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka akipokea vitambulisho 6000 kutoka kwa H.Kitukuro -Kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw.Emmanuel Sukums vitambulisho 6000 vya wajasiriamali
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw.Emmanuel Sukums Akikabidhii vitambulisho vya wajasiriamali kwa Afisa Tarafa ya Ngorongoro Bw.Bahati Mfungo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw.Emmanuel Sukums Akikabidhii vitambulisho vya wajasiriamali kwa Afisa Tarafa ya Loliondo Bw.William Ndossi
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.