Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Mfaume Taka akabidhiwa miradi mitatu na wadau wa maendeleo na Bodi ya Focus on Tanzanian Communities (FoTZC)kwa ushirikiano wa kampuni ya Thomson Safaris Ltd katika kijiji cha sukenya kata ya Oloipiri Wilayani Ngorongoro.
Kabla ya ya makabidhiano hayo Mh.Rashid Taka alipata nafasi ya kuzungumza na bodi ya Focus on Tanzanian Communities (FoTZC) iliyoongozwa na Bi Bonny ambaye ni Rais wa bodi hiyo na kutembelea miradi yote mitatu ikiwemo nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Sukenya,nyumba ya walimu katika shule ya msingi mondorosi na borehole katika kijiji cha mondorosi.
Mkuu wa wilaya ameongeza kwa kusema kuwa serikali ya awamu ya tano inajali na kutambua juhudi za mashirika na wadau wa maendeleo kwa kuchangia miradi ya maendeleo hasa kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya hivyo serikali ipo tayari kuonyesha ushirikiano ili kusaidiana kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
Sambamba na hayo amewashukuru wananchi wa kijiji cha Sukenya na Mondorosi pamoja na Kampuni ya Thomson Safaris Ltd, kwa ushirikiano wa Focus on Tanzanian Communities (FoTZC) katika kutekeleza miradi hiyo kwaajili ya maendeleo na kuwaahidi ataendelea kutoa ushirikiano na kuwaomba kusaidia tena ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Sukenya pamoja na madarasa manne katika shule ya msingi Mondorosi.
Kwa upande wake Rais wa bodi ya Focus on Tanzanian Communities (FoTZC)Bi Bonny, amewashukuru wanachi wa kijiji cha Sukenya na Mondorosi kwa kuonyesha ushirikiano na moyo wao wa upendo na kuwaahadi kuwa maombi yao wameyachukuwa na kwenda kujadiliana ili kupatiwa uvumbuzi.
Imetolewa na
Kitengo cha Habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Bi Elizabeth-Mwakilishi wa Miradi ya Focus on Tanzanian Communities (FoZTC)akiwa atambulisha wageni kutoka Bodi ya Focus on Tanzanian Communities (FoZTC kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka baada ya kuwasili katika Kijiji cha Sukenya.
Rais wa Focus on Tanzanian Communities (FoTZC)akimkabidhi Mh.Rahid Taka kibao kama Ishara ya Mkabidhiano ya Nyumba ya Watumishi katika zahanati ya Sukenya.
Picha ya pamoja kati ya Bodi ya Focus on Tanzanian Communities (FoTZC),Viongozi wa kata ya Oloipiri na viongozi wa wilaya ya Ngorongoro wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jengo la watumishi katika Zahanati ya Sukenya.
Bi Bonny Rais wa (FoTZC)akikabidhi kibao kwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Mfaume Taka kama ishara ya makabidhiano ya nyumba ya mwalimu katika shule ya Msingi Mondorosi
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh.Rashid Taka akikabidhi cheti cha Pongezi kwa Bi.Bonny Rais wa (FoTZC) baadha ya kufadhili ujenzi wa nyumba ya watumishi katika Zahanati ya Sukenya na Shule ya msingi Mondorosi pamoja na Borehole katika kijiji cha Mondorosi
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.