Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Kanali. Wilson Sakulo leo tarehe 24 Februari, 2024 ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na KFW, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya Kanali. Sakulo ambapo atakua na ziara maalum ya siku nne ya kutembelea miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Wilaya ya Ngorongoro.
Kanali. Sakulo ametembelea Shule ya Mama Silivia iliyopo mtaa wa Njorieti kukagua madarasa mawili yanayojengwa na KFW ambayo yako katika hatua ya umaliziaji yenye thamani ya Shilingi 100, 258, 000, na kutoa rai kwa wahisani hao kujenga miundo mbinu ya maji katika shule hiyo ili kuondoa uhaba wa maji.
"rai yangu kwenu ningependa mjenge miuondo mbinu ya maji kama kisima ili kuondoa changamoto ya maji katika Shule hii" amesema Kanali. Wilson Sakulo
Wakati wa ziara hiyo, Kanali. Sakulo ametembelea miradi ya barabara ya Mairowa mpaka Njoroi yenye urefu wa kilomita 11.1 ambayo iko katika hatua ya umaliziaji barabara hiyo imetengewa bajeti ya shilingi bilion 1.987, kisha kukagua barabara ya Kirtalo yenye urefu wa kilomita 12.5 inayotarajia kukamilika tarehe 6 April, 2024.
Hata hivyo Kanali. Sakulo ametembelea Shule za Sukenya iliyopo kata ya Oloipiri yenye madarasa matatu yenye thamani ya shilingi 211,905,100.70 ambayo iko katika hatua ya umaliziaji, Zahanati ya Njoroi yenye thamani ya shilingi 358, 803, 250.48, Shule ya Msingi Soitsambu yenye vyumba vitatu vya madarasa kisha kumalizia ziara kwa kukagua Zahanati ya Kirtalo yenye thamani ya shilingi
milion 358, 803, 250.48.
Kanali Wilson Sakulo amehitisha ziara yake kwa kuwahimiza wahisani wa KFW kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kuikabidhi ili jamii na Wananchi wa Ngorongoro waanze kunufaika maramoja
Hata hivyo Kanali Sakulo ametoa shukrani kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha mahusiano mazuri na mataifa mengine na kuruhusu Wahisani kuja nchini na kufanya miradi ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.