MKUU WA WILAYA YA NGORONGORO AZINDUA ,KAMPENI YA FURAHA YANGU KATA YA SAMUNGE"Pima Jitambue Ishi"
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mh Rashid Mfaume Taka amezindua kampeni ya FURAHA YANGU katika kata ya SAMUNGE ambayo inatembea na kauli mbiu isemayo "Pima Jitambue Ishi"Hata hivyo amewasihi WANAUME kushiriki ipasavyo katika zoezi la Upimaji wa magonjwa Mbalimbali ikiwemo UKIMWI na kusisitiza kuwa Huduma hiyo inatolewa Bure na wataalamu wa Afya kwa muda wa siku Tano tu.Pia amewasihi wananchi wa kata ya Samunge kujiunga na na Mfuko wa Bima ya afya ambayo kaya ya watu 6 itatibiwa kwa Shilingi elfu 15000 tu kwa mwaka.Wakati wa zoezi hilo alipokea wanachama wapya Kumi na nane wanaojiunga na Mfuko wa Bima ya Afya
Dc Taka akipokelewa na Viongozi wa kata ya Samunge baada ya Kuwasili
Mh Rashid Taka akiambatana na Mh.Kajurusi Stivin Diwani wa kata ya samunge na Bw.Benezeth Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ngorongoro Kukagua vibanda vya Kutolea huduma mbalimbali za kupima Afya
Mh Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro akiburudika na kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza katika kampeni hiyo
Mh Rashid Taka alifungua Kampeni ya FURAHA YANGU kATIKA KATA YA SAMUNGE"Pima Jitambue Ishi" kwa kuwahutubia wananchi
Viongozi mbalimbali wa kata ya Samunge na Wataalamu wa Afya wakiwa na Mh.Rahid Taka Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro (Mgeni Rasmi)Kwenye Jukwaa Kuu
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.