Mwenge wa Uhuru Leo tarehe 25 Julai, 2024 umekimbizwa wilayani Ngorongoro umetembelea miradi zaidi 8 yenye thamani ya shilingi bilioni 10.83 iliyopo katika kata ya Engarasero, Sale, Maalon, Samunge, Olorien Magaiduru na Kata ya Orgosorock
Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru zimeongozwa na Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava akiambatana na wakimbizaji wengine watano.
Mwenge wa Uhuru umeweka jiwe la msingi shule ya Msingin Monic kuzindua madarasa manne na matundu matatu ya vyoo, jiwe la msingi Zahanati ya Yasimdito, pia umezindua barabara ya kipambi yenye urefu wa kilomita 14.6, mradi wa wanafunzi wenye nahitaji maalumu Shule ya Msingi Mama Sara, ukiwemo mradi wa uwekezaji wa kituo cha mafuta Say Lopolun kisha mradi wa maji wa vijiji nane Kijiji cha ng'arwa wenye uwezo wa kuzalisha maji Lita milioni mbili kwa siku, pia imetoa cheti kwa klabu ya Wapinga rushwa katika Shule ya Msingi Monic.
Katika kudumisha na kuendeleza utunzaji wa Mazingira kama kauli mbiu ya mwenge inavyohasisha Ndg. Godfrey amepatmnda mti katika Zahanati ya Yasimdito
Hata hivyo Kiongozi wa mbio za Mwenge Ndg. Godfrey Eliakimu Mnzava ametoa rai kwa Wilaya ya Ngorongoro kulipa kipaumbele suala la uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye kila mikutano ya Wananchi itakayofanyika.
Ikumbukwe Wilaya ya Ngorongoro imepokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Karatu ambapo katibu Tawala Wilaya ya Ngorongoro Ndg. Hamza H. Hamza ameupokea Mwenge wa Uhuru kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Mhe. Kanali Wilson Sakulo kutoka kwa Katibu Tawala Wilaya ya Karatu Ndg. Lameck Karanga.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.