MZUNGUKO WA KWANZA WA MBWAMWITU CUP 2018 MECHI NNE ZAPIGWA VIWANJA TOFAUTI
Ili kuibua vipaji kwa vijana na kutambua umuhimu wa uhifadhi Halmashauri ya wilaya Ngorongoro kwa udhamini wa wadau wa maendeleo shirika la GIZ wameanzisha mashindano ya mpira wa miguu maarufu kama ligi ya mpwamwitu Cup yenye ujumbe wa Wanyama Wetu /Mifugo wetu /Fahari yetu
Ligi hiyo inashirikisha timu kumi (10) kutoka tarafa ya sale na Loliondo na katika mechi za ufunguzi leo kundi A,Serengeti boys imeibuka mshindi nyumbani kwa jumla ya 2-1 dhidi Soit sambu fc,
Serengeti boys ni ya kwanza kupata goli mnamo dakika ya 32 kupitia kwa mchezaji wake Lolusu, na Soitisambu FC kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji nuhu Ismail dkk ya 75, hata hivyo serengeti boys walijipatia goli la pili mnamo dakika ya 88 ya mchezo kutoka kwa super sub Leshan Kashe.
.
Kwingineko katika mchezo wa kundi B kulikuwa na mtanange kati ya mount lengai kutoka malambo dhidi ya digodigo home boys ambapo mbali na vijana wanyumbani Digodigo kuwa wenyeji wa michezo hiyo wamepokea kichapo cha goli 4-0 dhidi ya mount lengai.
Timu ya Soitsambu FC
Timu ya Serengeti Boys
Viongozi mbalimbali na waamuzi wakiwa katika mazungumzo mafupi kabla ya mechi kati ya Serengeti Boys na Soitsambu FC kuanza
Wachezaji wa SERENGETI BOYS wakifanya mazoezi kabla ya mechi kuanza
Soitsambu FC wakijadiliana jambo wakati
Timu ya SERENGETI BOYS wakati wa mapumnziko baada ya kupata goli la kwanza
Keptain wa Timu ya Soitsambu
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.