Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ngorongoro Mheshimiwa Wiliam Ole Nasha amekuwa neema kila alipotembelea wakati wa ziara yake katika tarafa ya Sale na Loliondo.
Akiwa tarafa ya sale Mh. Mbunge alitembelea vijiji vya Samunge, Digodigo, Mugholo, Kisangiro na Yasimdito.
Akihutubia wananchi katika kijiji cha Samunge mheshimiwa mbunge ameahidi million 70 za umaliziaji wa majengo ya kidato cha 5na 6 yaliyopo hatua ya lenta kwa muda mrefu pia millioni 7 kwa Kikundi cha malikia na rasheraniai. Mheshimiwa mbunge pia ameahidi nyumba ya walimu 2 in 1 katika shule za msingi za Rera na B isikene.
Kuhusu umeme amewaambia wananchi waliokusanyika kumsikiliza kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu kila kijiji cha Butemine kitakuwa kimeshapata umeme.
Kuhusu barabara amesema, barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami haitasimama bali inajengwa kwa awamu hadi ikamilike kuanzia Loliondo hadi Mto Wa Mbu.
Akizindua madarasa yaliyokarabatiwa katika shule ya msingi Yasimdito Mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia (MB) amesifu ukarabati wa madarasa uliofanyika akasema “ nimetoa milioni thelathini na sita (36) za kukarabati madarasa matatu badala yake mumekarabati manne na zimebaki million 7 na mumeanza jengo lingine, hongereni sana”. Amesema mradi huu wa milioni 36 ni wa mfano katika jimbo lake na atawatuma watu kutoka wizarani kuja kujifunza jinsi fedha kidogo inavyoweza kufanya mambo makubwa.
Kwa kufurahishwa na kazi iliyofanyika shule ya msingi Yasimdito mheshimiwa naibu waziri ameahidi kuwapatia million 50 kwa ajili ya kujenga nyumba ya walimu ya 2 in 1 na bati 80.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.