Katika siku ya tatu ya ziara yake, jumamosi ya tarehe 20/10/2018 mheshimiwa naibu waziri wa elimu sayansi na teknolojia na mbunge wa wilaya ya ngorongoro alitembelea kituo cha afya Sakala, maeneo ya Enguserosambu, Orkiu na kuhitimisha katika viwanja vya Loliondo Mjini.
Katika ziara hiyo ya kawaida jimboni, mheshimiwa Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na mbunge wa Wilaya ya Ngorongoro alihutubia wananchi katika maeneo mbalimbali aliyoyatembelea.
Akiwa katika Shule ya Msingi Enguserosambu, Mheshimiwa naibu waziri alizindua madarasa matatu na choo matundu 6 yaliyojengwa kwa fedha za EP4R. Aidha baada ya kusikiliza kero mbalimbali zinazoikabili shule hiyo hasa upungufu mkubwa wa nyumba za walimu naibu waziri amewaahidi kuwapatia millioni hamsini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba moja ya walimu wawili (2 in 1) katika shule hiyo. Mheshimiwa naibu waziri pia ameahidi kujenga madarasa matatu katika shule mpya ya msingi ya Lopiriki .
Akihutubia wananchi katika viwanja vya shule ya msingi Enguserosambu, Mheshimiwa mbunge amefurahishwa na jinsi wananchi wanavyosimamia miradi ya maendeleo akitolea mfano ujenzi wa madarasa matatu aliyoyazindua katika shule hiyo. Aidha amewataka wananchi kujitolea ili kujiletea maendeleo.
Kuhusu elimu, mheshimiwa Olenasha aliwataka wananchi kuwapeleka shule watoto wote wenye umri wa kwenda shule na kwa wale watakaofaulu kwenda sekondari wazazi wahakikishe wanawapeleka shule watakazopangiwa. Alisisitiza kuwa hatamvumilia mzazi yeyote atakayeshindwa kumpeleka mtoto sekondari kwani Elimu inatolewa bila malipo.
Naye mwenyekiti wa halmashauri mheshimiwa Mathew Siloma akihutubia mkutano huo ameagiza kikundi cha wakinamama cha Naserian cha Naan kipewe shilingi million 4 kutoka Halmashuri.
Kero zingine zilizojitokeza katika mikutano yake ni kero za umeme na maji ambapo ameahidi kuzifuatilia na kuzipatia ufumbuzi. Kuhusu umeme mheshimiwa naibu waziri amewataka wananchi kijiandaa kupokea mradi mkubwa unoendelea kujengwa wa umeme wa REA.
Mheshimiwa William Olenasha akikagua Moja kati ya Majengo Manne yaliyojengwa Katika Kituo cha afya Sakala
Hapo juu Vyumba vitatu vya Madarasa na Choo Matundu sita yaliyojengwa katika Shule ya msingi Enguserosambu
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.