Halmasahuri ya Wilaya ya Ngorongoro imeendelea na utekelejazi wa agizo lakufanya usafi kila jumamosi ya Mwisho wa mwezi .
Agosti 26,2023 wananchi mbalimbali katika Vijiji na Mitaa ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro wamejitokeza kufanya usafi kwenye maeneo yao ya makazi .
Akizungumza Mara baada ya usafi huo Bw.Mpoki Afisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro amesema niutaratibu ambao wameuweka wakuhakikisha wananchi wanafanya usafi katika maeneo yao ya makazi na mahali wanapofanyia Biashara ili kuepuka na magonjwa ya Mlipuko yanayoweza kutokea .
Timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro ilishiriki Pamoja na wananchi kufanya usafi katika mtaa wa Wasso kwenye Mamlaka ya Mji mdogo wa Loliondo
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.