Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kimefanyika leo tarehe siku ya Jumatatu tarehe 30.1.2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Akizungumza wakati wa ufunguzi Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw Emanuel Mhando amewataka wajumbe kushiriki kikamilifu kwa kutumia Fursa hiyo muhimu kujadili Hoja zitakazojitokeza ili kufanikisha shughuli mbalimbali za Halmashauri
Katika kikao Hicho wajumbe walifanya Uchaguzi wa Kumchagua katibu wa Baraza la wafanyakazi ambapo Wagombea Ndg.Lawrance Ledio aliibuka mshindi kwa kura 34 na Kuwa katibu wa Baraza la Wafanyakazi dhidi ya Fausta Bura aliyepata Kura 23 na kuwa katibu msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi.
Katika Kufikia Malengo ya Kikao hicho wajumbe wamepata Fursa ya Mafunzo na Kujadili mada ya Mapitio ya Bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Baraza la wafanyakazi ni Baraza ambalo lipo kwa mujibu wa Agizo la Rais Na.1 la mwaka 1979 ambalo lina lengo la kuwashirikisha wafanyakazi wa Ngazi zote katika utekelezaji wa shughuli za Taasisi kwa kushirikiana na Uongozi.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.