"Napenda kuishukuru serikali ya awamu ya sita, chini ya mama yetu wa taifa Dk. Samia Suluhu Hassan rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kupitia wizara ya afya, elimu na ofisi ya rais TAMISEMI pamoja na wadau wote wa programu mbalimbali za usafi na mazingira, ambao wamekua ni sehemu ya kufanikisha kutokomeza magonjwa yanayosababishwa na hali duni ya usafi wa mazingira"-Mhe Raymond Mwangwala DC wilaya ya Ngorongoro.
Ametoa shukrani hizi wakati akifungua kikao cha programu ya maji, usafi na mazingira vijijini (SRWSS). kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro, kilichohudhuriwa na viongozi wa vijiji, madiwani, watendaji wa kata na viongozi wa dini kata ya Digodigo, Orgosorok, Samunge, na Namholo.
Aidha mhe. Raymond Mwangwala amewasisitiza viongozi hawa kuwakumbusha wananchi kuzingatia usafi ili kuepuka magonjwa yatokanayo na uchafu. Pia serikali kupitia wizara ya ofisi ya rais TAMISEMI imetoa kiasi cha shilingi 339,277,830 kwa halmashauri ya Ngorongoro kwenye sekta ya afya na elimu kwa lengo la kuboresha miundo mbinu ya usafi wa mazingira.
Ikiwemo miundo mbinu ya vyoo vya magonjwa ikiwemo vyoo wa wagonjwa wenye mahitaji maalum, vyoo vya wanafunzi wa shule za msingi, kuboresha, kuimarisha usafi wa mazingira katika kaya na kuhakikisha wananchi wanajenga vyoo bora.
Aidha mkuu wa wilaya ametoa wito kwa vyombo vya habari, wananchi, viongozi wa jamii kuhakikisha wanapeleka ujumbe kwa jamii na kuwaelimisha, kuwaelekeza kujenga na kutumia vyoo bora.
Pia mhe Raymond Mwangwala ametoa agizo la utekelezaji wa mradi huu wa ujenzi wa vyoo vya kisasa uanze kutekelezwa mara moja na kufikia tarehe 13 Novemba 2023 uwe umekamilika.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.