Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenan Laban Kihongosi @kenanikihongosi amewasili kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa huo na kupokelewa kwa nderemo na vifijo na wakazi wa mkoa wa Arusha wakiwemo viongozi wa Chama na Serikali, viongozi wa dini, watumishi wa Umma, wadau wa maendeleo wa mkoa huo, wakiongozwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo aliyemaliza muda wake Ndugu Paul Christian Makonda.
Mhe. Kihongosi amepata wasaa wa kusalimiana na kuzungumza na wakazi wa Arusha muda mfupi kabla ya kukabidhiwa rasmi Ofisi mapema leo Juni 30,2025
Karibu Arusha Mhe.Kihongosi, tuko tayari kwa kaziā
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.