RS ARUSHA
Mkuu wa mkoa ameuagiza uongozi wa wilaya ya Ngorongoro kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa manne ya shule ya msingi Ololosokwani, madarasa yanayojengwa na serikali kupitia mradi wa BOOST.
Mhe. Mongella ametoa maagizo hayo mara baada ya kukagua mradi huo na kukuta bado hayajakamilika na kuwataka viongozi hao kuhakikisja kabla ya tarehe 10.12.2023 kukamilisha ujenzi huo kwa kuweka milango, marumaru, meza na viti vya walimu pamoja na madawati 60 ikiwa madawati 15 kwa kila darasa.
"Mkuu wa wilaya na mkurugenzi hakikisheni, mnakamilisha miradi hii kwa kutumia fedha zilizotolewa na serikali kwa kuwa fedha hizo zimekuja na maelekezo ya kukamilisha mradi, kuweni na tabia ya kufuatilia utekelezaji wa miradi hatua kwa hatua, msikubali fedha kumalizika kabla ya mradi haujakamilia" Amesema Mhe. Mongella.
"Kabla ya tarehe 15 Desemba majengo yote yawe yamekamilika, wekeni milango, pakeni rangi, wekeni 'tiles' pamoja na samni zote, viti na meza za walimu, madawati 15 kila darasa, nikirudi nikute vitu vyote vimefanyika, Mkurugenzi fuatilieni kwa karibu" Amesisistiza Mkuu huyo wa mkoa.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Mwalimu mkuu shule ya msingi Ololosokwani, Mwl. Luciana Labi Manya amesema, mradi huo umetekelezwa na Serikali kupitia mradi wa BOOST kwa gharama ya shilingi milioni 106.3
Amefafanua kuwa kiasi hicho cha fedha, kinajumuisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, matundu matatu ya vyoo, meza na viti vya walimu kwa 1madarasa yote pamoja na madawati 60 madawati 15 kwa kila darasa.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.