Na Gabriel E. Mpeho
20 July 2023
Mtandao wa Wafugaji Tanzania (TPCF)limetoa mafunzo kwa wazee wa kimila(malaigwanani na mamije) juu ya umiliki ardhi kimila .
Mafunzo hayo yanalengo pia la kuwajengea uelewa malaigwanani hao na kutoa fursa pia kwa wanawake jamii za kifigaji kupata fursa kwaajili ya kumiliki ardhi na mifugo badala ya kutengwa .
Akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na TPSF jana Wilayani Ngororongoro Mkoani Arusha,Ofisa Tarafa ya Loliondo,William Ndosi alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa malaigwanani hao ili kuwajengea uelewa wa umiliki wa ardhi kisheria hususan ardhi za kimila.
Alisema serikali imepima maeneo wilayani humo lakini sasa taratibu zinazofatiwa ni kila aliyepimiwa ardhi hiyo apate hati miliki yake kisheria.
"Maeneo Ngorongoro yamepimwa na muda wowote kuanzia sasa serikali itatoa hati miliki ya kimila hivyo wazee wa kimila na wanawanamije tuungane kwa pamoja kuhakikisha wanawake nao wanapata haki ya kumiliki ardhi na mifugo "
Naye Mkurugenzi wa TPCF,Joseph Parsambei alisema shirika hilo linatoe elimu juu ya umiliki wa ardhi kwa viongozi wa mila ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhalali wa umiliki ardhi ya kimila.
Alisisitiza shirika hilo kuendela kushirikiana na serikali katika kuhakikisha mambo mbalimbali yanafanikiwa ikiwemo wanawake kumiliki ardhi
Huku mmoja kati ya malaigwanani walioshiriki mafunzo hayo kutoka kata ya Olorien Magaiduru alisema mafunzo hayo ni muhimu kwao katika kuondoa mfumo dume wa kuwabagua wanawake kumiliki ardhi au mifugo katika jamii za wafugaji.
Aliomba shirika hilo kuendelea kutoa elimu zaidi kwa jamii hiyo ili wanawake nao waweze kujikwamua kiuchumi.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.