Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro imepokea vifaa maalumu kwaajili ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania imeendelea kuipa kipaumbele sekta ya Elimu nchini kwa kutoa vifaa maalumu vitakavyokwenda kuwasaidia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Endulen
Aidha vifaa hivyo vimepokelewa katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bw. Emmanuel Mhando akiwa na Madam Mwanamina Muro Afisa Elimu Awali na Msingi Wilaya, Mwl. Ronald Mwende Afisa Elimu Maalum Wilaya, pamoja Mwl. Hamad Lesso Mkuu wa Shule ya Msingi Endulen
Hata hivyo Bw. Emmanuel Mhando kwaniaba ya uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro amemshukuru Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuamua kutoa vifaa hivi maalumu kwaajili ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwani vinakwenda kuleta tija kubwa katika Sekta ya Elimu hapa nchini.
Ikumbukwe lengo la vifaa hivi ni kuchochea maendeleo ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika ufaulu, kutokomeza utoro pia kuimarisha na kuboresha Sekta ya Elimu maalumu Wilaya ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.