LOLIONDO ,ARUSHA
Halmashauri kuu ya CCM katika kikao chake imewatunuku vyeti vya Pongezi kwa Shule za Sekondari zailizofanya Vizuri katika Mitihani ya Kitaifa 2018 ya Kidato cha pili kidato cha nne na Kidato pili
Aidha katika shule iliyoibuka kwa Kufanya Vizuri katika Mitihani ya Kidato cha sita nafasi ya Kwanza ni Embarway Sekondari,nafasi ya Pili ni Loliondo Sekondari na nafasi ya Tatu ni Nainokanoka Sekondari kati ya Shule Tatu za Kidato cha sita zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Akizungumza katika kikao hicho ,Naibu waziri wa Waziri WA Elimu na Sayansi na Tekinolojia Mh.William Olenasha Ambae pia ni Mbunge wa Ngorongoro amezipongeza shule zote zilizofanya Vizuri na Kuahidi kutoa zawadi kwa shule ambazo zitafanya Vizuri katika Kuteleleza na kusimamia vizuri Miradi ya Maendeleo
Wakati wa Ugawaji wa tuzo hizo kaimu Mkurugenzi Mtendaji Bw.Peter Juma ameeleza kuwa shule hizo wamezipanga katika makundi tofauti kulingana na Ushindi wa nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika Mitihani ya Kitaifa ya kidato cha pili ,Kidato cha nne na kidato cha sita
Pia katika Mitihani ya Kitaifa ya Kidato cha 4 shule iliuokuwa kinara ni Sale Sekondari imeshika nafasi ya Kwanza ,Shule ya Sekondari Lake Natron Nafasi ya Pili kifwatia na Nafasi ya Tatu ni Shule ya Sekondari Loliondo kati ya Shule kumi na moja za sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Katika Mitihani ya Kidato cha Pili shule ya Sekondari Loloondk imeibuka kididedea kwa kushika nafasi ya Kwanza kufwatiwa na Shule ya Sekondari Arash na Nafasi ya Tatu imeshikwa na Shule ya Sekondari Emanyata kati ya Shule kumi na Moja za sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Aidha Shule ya Sekondari Arash pia ilipata Cheti cha Pongezi kwa kuwa shule zinazoibuka kufanya Vizuri kulinganisha na Matokeo yake ya Mwaka 2017
Imetolewa na Kitengo
Habari na Mawasiliano
Hakmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.