TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI UDAHILI MWEZI MARCH 2019
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDITAARIFA KWA UMMA KUHUSU MAOMBI YA UDAHILIKWA MUHULA WA MACHI, 2019
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheriaya Bunge Sura ya 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu yaufundi katika vyuo vinavyotoa mafunzo kwa ngazi za Astashahada, Stashahada naShahada ambavyo si Vyuo Vikuu au Vyuo Vikuu Vishiriki nchini. Mojawapo yamajukumu ya Baraza ni kuhakikisha kuwa mafunzo yanayotolewa katika Vyuo vyaElimu ya Ufundi yanakidhi vigezo na ubora unaohitajika katika soko la ajira ndani nanje ya nchi.Baraza linapenda kuufahamisha umma kuwa Udahili wa wanafunzi katika ngazi yaAstashahada na Stashahada kwa kozi zote isipokuwa Ualimu utaanza kutoka tarehe15 Januari, 2019 hadi tarehe 20 Februari, 2019. Udahili katika Muhula huu waMachi, 2019 utahusisha vyuo vyote vilivyo na nafasi na uwezo wa kupokeawanafunzi wapya. Vyuo vya Serikali vinavyotoa mafunzo katika sekta ya afyahavitahusika na udahili huu.Aidha, wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na Vyuo wenye sifa za kujiunga nakozi za Astashahada na Stashahada wanataarifiwa kutuma maombi yao yakudahiliwa moja kwa moja vyuoni. Waombaji watakao chaguliwa na vyuowatakavyomba watawasilishwa NACTE kwa ajili ya uhakiki kabla ya kufahamishwakujiunga na mafunzo. Masomo kwa watakaochaguliwa na kuhakikiwa yataanzatarehe 5 Machi, 2019.Baraza lina shauri vyuo na taasisi zote zitakazo dahili wanafunzi kwa Muhula waMachi, 2019 kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu za matukio ya udahili kamazilivyo kwenye Kalenda ya Udahili (Admission Calendar) inayopatikana kwenyetovuti ya Baraza.Pia Baraza linawashauri waombaji na wazazi kuhakikisha kuwa wanaomba kwenyeVyuo vilivyokidhi ubora ambavyo vimeorodheshwa kwenye Kitabu cha Mwongozowa Udahili kwa mwaka 2018/2019 (Admission Guidebook for 2018/2019).Mwongozo wa Udahili unapatikana katika tovuti ya NACTE: www.nacte.go.tz.IMETOLEWA NA:OFISI YA KATIBU MTENDAJIBARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)TAREHE: 11/01/2019
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.