Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega Leo Jumatatu Januari 06, 2024 akiwa Jijini Arusha kwenye Kikao cha Bodi ya barabara Mkoa wa Arusha, Ameagiza mamlaka zote zinazohusika na ufungaji wa Taa za barabarani nchini Tanzania kuachana na mifumo ya taa zinazotumia umeme na badala yake zifungwe taa zinazotumia nishati ya Jua ili kuondokana na gharama kubwa za uendeshaji wa Taa hizo za barabarani.
Mhe. Ulega ametoa tamko hilo ikiwa ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda aliyewasilisha kwa Waziri huyo pamoja na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba akiomba usaidizi katika ufungaji wa taa za barabarani zinazotumia nishati jua, ili kuondokana na gharama kubwa za uendeshaji wa Taa zinazotumia umeme.
Katika utekelezaji wake, Waziri Ulega ameiagiza Wakala wa barabara Mjini na Vijijini TARURA pamoja na Wakala wa barabara Tanzania TANROAD kushirikiana pamoja kuhakikisha Jiji la Arusha linafungwa taa kwenye maeneo yote muhimu ili Jiji hilo liweze kuwa na hadhi ya kuvutia zaidi watalii na mikutano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa pamoja na kuufanya Mkoa huo kuwa na hadhi ya kustahimili Ofisi nyingi za kidiplomasia zilizopo Jijini Arusha.
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.