Sale -Ngorongoro
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kupitia idara ya TASAF katika mpango wa kunusuru kaya maskini imekabidhi miradi sita kwa vikundi vya wakinamama na vijana katika kata ya sale wilayani Ngorongoro.
Lengo la mradi huo ni kunusuru kaya maskini chini ya Mpango wa kupunguza Umasikini ambayo mpaka sasa imewezesha wananchi wa Kijiji cha Sale kutekeleza miradi yenye kuleta tija kwa wananchi kama sehemu ya Mkakati wa Taifa wakupunguza Umasikini.
Akielezea miradi hiyo kwa Mgeni rasmi mratibu wa TASAF Wilaya Ngorongoro Bw. Luther Zablon amesema kijiji cha Sale kina jumla ya walengwa wa kaya maskini 354, ambao wapo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini na wamekuwa wakipata ruzuku ya msingi na masharti kwa lengo la kuakikisha watoto wanapata huduma ya kliniki na kuanzia miaka mitano kuhudhuria shule.
Kijiji cha Sale kilipata ufadhili wa miradi sita (6) kutoka TASAF III PSSN chini ya Mpango wa kupunguza Umasikini TPRP III unaofadhiliwa na OPEC III. Miongoni mwa miradi hii Mradi mmoja ni wa Umwagiliaji na Miradi mitano 5 ya Vikundi vya uzalishajimali, Vikundi viwili miradi ya ushonaji wa vyerehani, miradi miwili miradi ya ushonaji shanga na kikundi kimoja mradiwa mashine ya kusaga.
Akitaja miradi hiyo Bw. Zablon amesema wananchi wametekeleza mradi wa umwagiliaji uliogharimu kiasi cha shilingi 74,998,465.91.ikiwa ni pamoja na na fedha za usimamizi na aslimia moja na nusu (1.5) za kijiji.Mfereji huo wa umwagiliaji unakusudi la kupunguza tatizo la upotevu wamaji kabla ya kufika maeneo husika.
Pia ameeleza kuwa vikundi vya ushonaji kwa cherehani vimepatiwa vyerehani sita (6)kila kimoja na majora ya nguo kwa kuanzia na mafunzo mbalimbali kuhusu uendelevu wa vikundia ambayo ni zaidi ya milioni kumi kumi na tisa na yataendelea kutolewa na sekta kwa kushirikiana na wadau wengine na baadaye miradi hii itajitegemea.
Akizungumza na wanavikundi Mgeni Rasmi Bw.Emanuel Sukums,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro amewaeleza wanavikundi kutunza na kuzalisha miradi yote waliokabidhiwa ili ilete tija katika maisha yao
Pia amewaeleza kuwa ziada inayopatikana katika miradi hiyo iwasaidie katika maisha yao lengo ni kujikwamua katika wimbi la umasikini na amewataka viongozi kusimamia miradi yote ili iwe na manufaa kwa walengwa.Bw.Sukums alimalizia kwa kusisitiza wasimamizi wa mradi ikiwa vikundi husika wakisaidiana na wataalam washauri kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ngorongoro.
Imetolewa na Idara ya Habari na Maelezo
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.