TIMU NNE ZAINGIA NUSU FAINALI YA MBWA MWITU CUP 2018
Ngorongoro, Arusha
Jumatatu 12,November 2018
Ligi ya mbwamwitu cup imefikia katika hatua ya robo fainali baada kushuhudia timu nyingine mbili kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ambazo zinaungana na timu ya Mount Lengai kutoka Malambo na Home boys FC kutoka Digodigo zilizotangulia kufuzu hatua hiyo.
Timu ya Kurugenzi FC ambao, walikuwa nyumbani kuwakaribisha White Flamingo wameibuka kidedea baadaa kupata ushindi wa jumla goli 2-1 na kujipatia tiketi ya kufuzu kucheza nusu fainali katika mashindano haya.
Mchezo huo ulikuwa wa vuta nikuvute ambapo timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu,na hatimaye Kurugenzi FC wakapata goli la kwanza kunako dakika 38 ya mchezo lililofungwa naye Gabriel Mwaikombe, na hadi kipindi cha kwanza kinakamilika Kurugenzi FC walienda mapumziko wakiwa na goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa mshikemshike hadi dakika ya 50 ya mchezo ambapo White Flamingo walipata penat,na kupata goli la kwanza na la kusawazisha.
Matokeo hayo yalidumu hadi kunako dakika ya 81 ya mchezo ambapo Kurugenzi FC walijipatia goli la pili kupitia mwiba mkali yuleyule Gabrel Mwaikombe akirudi nyavuni na kupachika goli hilo la ushindi.
Na matokeo hayo yalitosha kufanya timu ya Kurugenzi FC kujiandikia tiketi ya kucheza nusu fainali katika mashindano haya,huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngorongoro Ndugu Raphael Siumbu akishuhudia Mchezo huo.
Katika mchezo mwingine wa kufuzu hatua ya kufuzu kucheza nusu fainali ilikuwa kati ya Nyuki Rangers ambao walikuwa wenyeji kwa kuwaakaribisha Loliondo FC na tukishuhudia Loliondo wakifuzu kucheza nusu fainali kwa kuifunga Nyuki Rangers mbali na kuwa yumbani kwa jumla ya goli 2-1 huku magoli ya Loliondo yakifungwa na Ally Ngoma na Halid Wantala na mchezaji Fanuel Andrea akifungia Nyuki Rangers goli moja kwa njia ya penati.
Matokeo hayo yanafanya timu hizo ya Loliondo FC, Kurugenzi FC na Mount Lengai FC pamoja na Home Boys kukutana katika hatua ya nusu fainali wiki ijayo tarehe 17 na 18 -11-2018
Imetolewa na
Kitengo cha habari na Uhusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mchezaji wa Kurugenzi FC Bwana Gabriel Mwakiombe akinyanyuliwa Juu kwa furaha na mashabiki wa Kurugenzi FC baada ya kuifungia timu yake jumla ya mabao mawili dhidi ya White Flamingo FC katika viwanja vya Wasso Shule ya Msingi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Raphael Siumbu akizungumza na wachezaji pamoja na mashabiki baada ya Mchezo baina na ya Kurugenzi FC na White Flamingo kumalizika katika viwanja vya wasso shule ya msingi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Raphael Siumbu akisalimiana na Dr.Kunei aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngorongoro (Mstaafu) katika viwanja vya shule ya Msingi Wasso
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Bw.Raphael Siumbu akitazama mchezo baina ya Kurugenzi FC na White Flamingo katika viwanja vya shule ya msingi Wasso
Kikosi cha Timu ya White Flamingo FC wakiwa tayari kuanza mchezo baina ya Kurugenzi FC
Kikosi cha Timu ya Kurugenzi FC wakiwa tayari kuanza mchezo wa kukabiliana na kikosi cha timu ya White Flamingo ya Pinyinyi
Hakimiliki©2017 NDC . Haki zote zimehifadhiwa.